Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo, Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar, Sadifa Juma.
NA WAANDISHI WETU
Risasi Jumamosi
DAR ES SALAAM: Makubwa! Aliyekuwa mume wa nyota wa Filamu za Bongo,
Wastara Juma ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Donge (CCM), Zanzibar,
Sadifa Juma ameibua jambo zito miongoni mwa jamii akidai kuwa, mtalaka
wake, Wastara Juma amekuwa akimroga, twende na Risasi Jumamosi.
Madai hayo aliyatoa Alhamisi iliyopita baada ya gazeti hili kumuuliza
habari zilizoenea kwamba, amemuangukia Wastara akitaka warudiane kwani
yaliyopita si ndwele.
Sadifa alisema kuwa, aligundua hilo la kurogwa baada ya Wastara kuondoka
nyumbani kwake na kutangaza kwenye vyombo vya habari kuwa, amepewa
talaka mbili.
Akizungumza kwa dakika 25, Sadifa
alikwenda mbele zaidi kwa kusema: “Ukimwangalia Wastara harakaharaka
unaweza kusema ni mwema sana lakini hana wema wowote. Hivi Wastara ni wa
kuniroga mimi kweli?”
Wastara Juma akiwa na aliyekuwa mumewe, Sadifa Juma siku ya ndoa yao.
Wastara Juma akiwa na aliyekuwa mumewe, Sadifa Juma siku ya ndoa yao.
ILIKUWA HIVI
Risasi Jumamosi: (baada ya kujitambulisha na salamu) “mheshimiwa tunataka kujua nini kinaendelea kati yako na mkeo Wastara?”
Mume: “Kuhusu nini?”
Risasi Jumamosi: “Kuna madai kwamba, umeamua kumrudia na wiki
iliyopita uliwapa gari mashemeji zako waende Morogoro kumfuata Wastara.”
Mume: “Kwanza hizo habari si za kweli. Mimi wale mashemeji zangu
waliniomba gari wamfuate ndugu yao. Nilitoa kwa ubinadamu tu,
nikawawekea na mafuta.”
AMTAJA RAFIKI WA SAJUKI
Risasi Jumamosi: “Lakini inadaiwa kuwa ulisema arudi mkae myamalize, ila
kule Morogoro kwa yule babu yake, ikawa kazi kutoka, unasemaje kuhusu
hilo?”
Mume: “Babu yake yupi?”
Risasi Jumamosi: “Yule Abdulaaziz Babu.”
Mume: “Yule si babu yake Wastara. Yule ni bwana’ake kama hamjui. Mimi
juzi tu ndiyo baadhi ya ndugu zake wameniambia ukweli kwamba yule babu,
si babu yao bali alikuwa rafiki mkubwa wa marehemu Sajuki (Juma
Kilowoko, aliyekuwa mume wa Wastara).”
ASEMA AMEMCHUKULIA MKE
Sadifa hakuishia hapo, aliendelea kumwanika Wastara hivi:
“Sasa wewe jiulize, mkeo mnagombana, anakwenda kwa rafiki wa marehemu
mume wake. Kwa nini asiende kwao? Kule anakaa kufanya nini? Yule Babu
ndiye amenirithi mimi kwa Wastara.”
AFUNGUKA ZAIDI
“Kuna wakati fulani Wastara aliumwa, dokta akamwambia atulie kwa muda
asitembeetembee. Kesho yake akaniambia anakwenda Morogoro kwa huyo babu
yake. Nilimkatalia, akalazimisha, akaenda. Sasa mke anawezaje kwenda
mahali bila ridhaa ya mumewe?
Wastara Juma
“Alipokuwa kule, nikawa nampigia simu hapokei kwa muda wa siku tatu.
Siku moja nyumbani alikuja kijana wake anayemfanyia biashara,
nikamwambia Wastara yupo Morogoro, akampigia simu mbele yangu, akapokea,
wakaongea. Walipomaliza, mimi nikampigia, hakupokea!”
BABU ALIOMBA PESA KWA MUME
“Basi, siku hiyo huyo babu akanipigia simu, akasema eti Wastara anaumwa,
mguu unatoka damu, nimtumie pesa ampeleke hospitali. Nikamwambia sina
na hata kama ningekuwa nazo nisingetuma.
KUHUSU KUMROGA
“Hivi Wastara ni wa kuniroga mimi kweli?”
Risasi Jumamosi: “Kukuroga? Hayo sasa ni mambo ya imani mheshimiwa. We umejuaje kama anakuroga?”
Mume: “Niliambiwa na watu wawili, mmoja dereva wangu, mwingine ni kijana
wangu. Tena hao wameniambia juzi tu baada ya mambo kuharibika.
ADAI KUTEGEWA KOMBE
“Wakasema kuna siku walikwenda na Wastara kwa huyo mganga. Wastara
alikuwa na ndugu yake mmoja. Walipofika, vijana wangu hawakuingia. Kwa
hiyo hawakujua walifuata nini! Mara ya pili akawaambia kuwa, wamekwenda
pale kuchukua dawa eti ili isaidie ndoa yetu iwe na amani na mimi niache
macho juujuu. Akapewa kombe kama unalijua kombe, aitie kwenye maji
anipe ninywe.
“Sasa wale vijana wangu wakamshauri Wastara kwamba, kama maji hayo ya
kombe atanipa yeye ninywe nikigundua itakuwa balaa, wakamwambia awape
wao ndiyo wanipe mimi ninywe ili nikijua wataniambia ni dawa ya kukinga
mwili. Lakini wao hawakunipa na wanayo mpaka leo (juzi, Alhamisi)!”
SIKU YA WASTARA KUONDOKA NYUMBANI
“Mimi sikuwahi kutoa talaka kama Wastara anavyoeneza hizi habari. Siku
hiyo anaondoka nyumbani mimi nilikwenda kwenye kamati za bunge, wakati
naingia akanipigia simu na kusema anataka tuongee.
“Nilimwambia tutaongea baadaye yeye akataka muda uleule, nikakataa.
Akasema anachotaka yeye nimpe shilingi milioni kumi afanye biashara.
Nikamwambia sina, ndiyo akaondoka. Sasa jamani, mkeo kama anataka pesa
ukamwambia huna ndiyo aondoke nyumbani? Mimi naona alifuata pesa tu.”
KUHUSU TALAKA SASA
Sadifa alizungumzia talaka ambapo alisema: “Sasa ndiyo nimeamua kumpa
talaka rasmi. Kesho (jana, Ijumaa) nitakwenda kwao kutoa talaka labda
wakimbie.”
BAADA YA MUME, WASTARA HUYU HAPA
Baada ya Sadifa kutumia dakika 25 kumzungumzia Wastara, naye mwanadada huyo akatumia dakika 22 kujibu mapigo.
AANZA KWA MADAI YA KUROGA
Wastara alisema kuwa, anajua mwanaume huyo atasema mengi yakiwemo hayo ya kumroga, lakini..:
“Lakini mimi sijamroga wala sina mpango huo. Kama hao vijana wake
wamemwambia hivyo, mbona vijana haohao waliwahi kuniambia kuwa, yeye
amewatuma wampigie picha mahali ili aseme amenifumania. Mimi nilisema
wapi!”
ANAPANGUA KUHUSU BABU
“Atasema mengi, mimi na babu hatuna chochote zaidi ya kuwa mtu wa
karibu. Yeye ana mangapi mimi sijasema. Mbona anakunywaga sana pombe.”
SH. MILIONI KUMI
“Kumuomba shilingi milioni kumi ni kweli. Na nilimwomba kwa kuwa ni mume
wangu, sasa ningemuomba nani. Na ni pesa ambayo aliniahidi toka siku
nyingi.”
KUMBE ALILAZIMISHWA KUOLEWA!
“Kwanza ngoja nikwambie, anaposema mimi nilifuata pesa kwake si kweli.
Mimi nimeishi na Sajuki katika maisha ya umaskini, sasa leo naanzaje
kufuata pesa kwa mtu. Ila mimi niliolewa kwa kulazimishwa, sikutaka
kuolewa na yule bwana.”
IWE KWA WEMA
Madai ya pande zote ni mazito. Hata hivyo, gazeti hili litaendelea
kufuatilia mwenendo wa wawili hao ili kujua mwisho wake. Lakini ushauri
kwa wote ni kukaa chini na kuondoa tofauti zao ili hata kama ni kuachana
iwe kwa wema na si kwa uhasama.
HUYU NI BABU
Gazeti hili juzi lilimpigia simu Babu ili kumsikia anasemaje kuhusu madai ya Sadifa. Yafuatayo ni maelezo yake:
“Kwanza nimecheka sana. Anaposema mimi nimemchukua mke wake aliniona
nyumbani kwake? Kwanza akumbuke wakati wa kumuuguza Wastara hivi
karibuni kwa nini aliniita nyumbani kwake? Kwa nini alikuwa akinipa gari
nimpeleke Wastara hospitali?
“Wakati anaondoka kwenda Zanzibar kwenye vikao vyao vya ubunge kwa
nini alikuwa ananiomba nimpeleke uwanja wa ndege (Dar)? Kama kweli yeye
haniamini kwa nini alikuwa anafanya yote hayo?
“Akae chini na Wastara waongee wayamalize. Mbona madogo sana hayo!
Asitumie ubunge wake kutisha watu. Kama anaamini mimi nimemchukua
Wastara achukue hatua yoyote ile.”